Main content

Imeandaliwa na Daniel Mwingira

Arusha. Vijana wenye ndoto za kuwa wajasiriamali wametakiwa kujituma na kuacha uoga ili kutumia vyema fursa zilizopo mbele yao kwa kuchangia kutatua matatizo yanayoikabili jamii.

Sisty Basil, Mratibu wa taasisi ya Energy Change Lab Tanzania alieleza wakati wa tamasha la Energy Safari 2018 lililofanyika jijini hapa kuwa vijana wengi wa Tanzania ni waoga wa kujaribu vitu na hata kujenga mtandao wa kibishara pale wanapopata nafasi ya kukutana na watu muhimu katika kuendeleza mawazo au biashara zao.

Kujituma, kujiamini na hamu ya kuongeza mtandao wa kujifunza na kufanya nao biashara ndiyo nguzo kwa kila mjasiriamali.

Tamasha la Energy Safari ambalo limefanyika kwa mara ya pili tangu kuanzishwa mwaka 2015, huwakusanya vijana  na kampuni mbalimbali zinazojihusisha na nishati mbadala hapa nchini. Katika tamasha la mwaka huu vijana 31 walifanikiwa kushiriki baada ya kufanikiwa kupita katika mchujo uliowahusisha waombaji 201 ikilinganishwa na waombaji 101 wakati linaanzishwa miaka mitatu iliyopita.

Sisty Basil, Mratibu wa taasisi ya Energy Change Lab Tanzania.

Basil amewataka vijana kuheshimu kila kitu wanachofanya na kutumia muda wao kwa ungalifu zaidi na kwamba matamasha kama Energy Safari ni njia bora ya kujenga mtandao mzuri wa kibiashara.

Bofya hapa kusoma zaidi, nakala imetayarishwa na Daniel Mwingirahttp://nukta.co.tz